6/recent/ticker-posts

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba Amekutana na Mshindi wa TUZO ya Chakula Duniani

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba (kulia), akipeana mikono na mshindi wa Tuzo ya Chakula Duniani ya mwaka 2026, Bw. Huub Lelieveld, walipokutana kwa mazungumzo katika ukumbi wa Iowa Events Center, jijini Des Moines, nchini Marekani, Oktoba 20, 2026.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba (kushoto), akimsikiliza mshindi wa Tuzo ya Chakula Duniani ya mwaka 2026, Bw. Huub Lelieveld (kulia), wakati wa mazungumzo yao katika ukumbi wa Iowa Events Center, jijini Des Moines, nchini Marekani, Oktoba 20, 2026.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba (katikati), akizungumza katika kikao na mshindi wa Tuzo ya Chakula Duniani ya mwaka 2026, Bw. Huub Lelieveld, kilichohudhuriwa pia na ujumbe wa Tanzania, katika ukumbi wa Iowa Events Center, jijini Des Moines, nchini Marekani, Oktoba 20, 2026.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefanya mazungumzo na mshindi wa Tuzo ya Chakula Duniani ya mwaka 2026, Bw. Huub Lelieveld, Oktoba 20, 2026, katika ukumbi wa Iowa Events Center, jijini Des Moines, nchini Marekani.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu amemweleza hatua zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha sekta ya kilimo. Aidha, amemwambia kuwa watafiti wa kilimo nchini Tanzania wanaendelea kujifunza kutokana na kazi zake ikiwemo uhifadhi wavyakula kwa njia za asili.

Bw.Lelieveld ni mwanasayansi kutoka Uholanzi anayejihusisha na masuala ya usalama wa chakula. Ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2026 na Taasisi ya Tuzo ya Chakula Duniani (World Food Prize Foundation).

Post a Comment

0 Comments