Na
Masanja Mabula, Pemba
Tatizo la akina baba kutoshiriki kikamilifu katika suala la chanjo kwa kufuatana na
akinamama kuwapeleka watoto kliniki kwa ajili kupatiwa chanjo, limedaiwa kuwa
moja ya sababu zinazozorotesha ufanisi wa zoezi hilo .
Ofisa
Tawala wilaya ya Wete, Mwalimu Khamis
Juma Silima, aliyasema hayo wakati akizindua wiki ya chanjo barani Afrika
ambayo kwa wilaya ya Wete yaliadhimishwa
katika kituo cha afya Kiungoni.
Aliwataka
akinababa kusimamia suala la chanjo kwa kuhakikisha wanaambatana na akinamama
kuwapeleka watoto kupatiwa chanjo katika vituo vya afya.
Katika
hotuba iliyosomwa kwa niamba yake na Ofisa
Utumishi Wilaya hiyo, Abdalla Ali Nuhu, Ofisa Tawala, alisema suala la
kuwapeleka watoto kupatiwa chanjo linawahusu wazazi wote katika familia.
Alisema
baadhi ya akinababa wamekuwa wakiwaachia jukumu la kuwapeleka kliniki watoto
akinamama hali ambayo inakwamisha kupatikana ufanisi.
"Akinababa
nao wanajukumu la kufuatana na akinama kuwapeleka watoto kupatiwa chanjo, kwani
kwa sasa bado wapo baadhi ya akinababa wanashindwa kutambua kuwa kufanya ni
hivyo ni wajibu wao kama wazazi,” alisema.
Aidha,
alisema ni vyema wananchi wakaitumia vyema fursa ya maadhimisho ya wiki ya chanjo
Afrika kwa kuhakikisha watoto wanaostahiki kupata chanjo hizo wanapatiwa kwa
wakati.
Naye
Ofisa wa afya wilaya hiyo, Dk. Ali Rashid Said, ameitaka jamii kuondoa dhana
kwamba chanjo hizo zinapunguza uzazi kwa watoto.
Alisema
serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kwa ajili ya kutoa huduma za chanjo kwa
wananchi wake, hivyo ni vyema wakajitokeza kwa ajili ya kuwachanja watoto wao.
Wiki
ya chanjo Afrika huadhimishwa kila ifikapo wiki ya mwisho wa mwezi Aprili kila
mwaka ambapo Mkuu wa kituo cha afya
Kiungoni, Dk.Hamad Khamis, aliwataka wazazi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo .
0 Comments