Na
Mwandishi wetu
RAIS
Jakaya Mrisho Kikwete, amekabidhi vitabu 2,181 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
kwa ajili ya vyuo vya jeshi ili kuongeza taaluma.
Rais
alikabidhi vitabu hivyo kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange na
kuahidi kuendelea kutafuta vitabu zaidi kwa ajili ya kuboresha maktaba ya jeshi
iliyopo katika Chuo Cha kijeshi kilichopo Monduli, Mkoani Arusha.
Maktaba
hiyo ilianzishwa na Rais Kikwete wakati alipokuwa mkufunzi katika chuo hicho
miaka iliyopita.
"Lazima
mtenge bajeti kwa ajili ya vitabu lakini na mimi nitaendelea kutafuta vitabu
niwaletee ili kuijengea uwezo maktaba yetu ya Monduli,” alisema.
Akipokea
vitabu hivyo kwa niaba ya Jeshi, Jenerali Mwamunyange alimshukuru Rais kwa
juhudi zake za kuboresha JWTZ kwa ujumla na kulifanya kuwa la kisasa zaidi.
“Juhudi
zako za kuliendeleza jeshi letu imetuongezea uwezo na kujiamini zaidi. Bila
juhudi zako tusingefika hapa tulipo na tunajivunia mafanikio haya,”alisema
Jenerali Mwamunyange.
0 Comments