Khamisuu Abdallah na Khamis Amani
Watu wawili wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Amani Abeid Amani Karume, wakisafirisha dawa za kulevya pipi 155 zenye uzito
wa 2.12kg kutoka Zanzibar kuelekea
Hongkong.
Watu hao walitambulika kwa majina ya Emmy Ambukage Mwaipaje
(39) na Ubwa Amani Muhamed (40) wote wakaazi wa jijini Dar es Salaam .
Vijana hao baada ya kukamatwa na dawa hizo walipandishwa
katika mahakama ya mkoa Vunga kusomewa mashitaka yao yanayowakabili.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka zilizowasilishwa mahakama
tofauti, Aprili 17 mwaka huu majira ya saa 10:00 za jioni washitakiwa hao
walikamatwa uwanja wa ndege wa Ameid Amani Karume wakiwa na dawa za kulevya
aina ya heroine.
Kosa la kusafirisha dawa za kulevya ni kinyume na kifungu 15
(1) (b) (1) sheria namba 9 kama ilivyofanyiwa
marekebisho kunyume na kifungu namba 11 cha sheria namba 12 ya mwaka 2011
sheria za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Emmy ambae alipandishwa katika kizimba cha hakimu Hamisuu
Saaduni Makanjira na kusomewa shitaka lake na Mwanasheria wa Serikali kutoka
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Anuar Khamis Saaduni, ilidaiwa
mwanamama huyo bila ya halali akiwa anasafiri kutoka Zanzibar katika uwanja wa
ndege wa Abeid Amani Karume kwenda Hong Kong
alipatikana na pipi 79 sawa kilogram
1.04 ambazo ni dawa za kulevya aina ya heroine.
Katika mahakama ya Hakimu Essaye Kayanje ambae ni Naibu Mrajis,
ambako alipandishwa mshitakiwa Ubwa na kusomewa shitaka lake na Mwanasheria wa
Serikali Omar Sururu, ilidaiwa alipatikana na pipi 76 swa na kg 1.08 ambazo ni
dawa za kulevya aina ya heroine.
Kosa la kupatikana na dawa za kulevya ni kinyume na kifungu
15 (1) (a) sheria namba 9 ya mwaka 2009 kama
ilivyofanyiwa marekebisho kinyume na kifungu namba 11 cha sheria namba 12 ya
mwaka 2011 sheria za kuzuia dawa za kulevya.
Washitakiwa hao wote walikataa mashitaka yao mbele ya mahakama hizo huku waendesha mashitaka
wakidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba kupangiwa tarehe
nyengine kwa ajili ya kutajwa.
Mahakimu wa mahakama hizo walikubalina na maombi ya upande
wa waendesha mashitaka huku Hakimu Hamisuu akiihairisha kesi ya mshitakiwa Emmy
hadi Mei 7 mwaka huu huku hakimu Essaya
akiihairisha kesi ya mshitakiwa Ubwa hadi Juni 8 mwaka huu na kuamuriwa
washitakiwa hao kurejeshwa rumande.
1 Comments
Usanii unaoneka dhahiri.Inakuwaje upelelezi usikamilike wakati washtakiwa wamekamatwa na kidhibiti?Au ndio mje mutwambie ni majivu?
ReplyDelete