Na
Madina Issa
UONGOZI
wa hospitali kuu ya Mnazimmoja umeelezea kusikitishwa na tukio la mtoto Mwanaidi Shukuru Mustafa (0.2) ambae amekatwa
mkono, wakati akipatiwa matibabu.
Tukio
hilo limetokeea
kutokana na tatizo la ‘gagril’ ambalo sio la makusudi inavyodaiwa na watu.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake, daktari kutoka kitengo cha watoto
katika hospitali hiyo, Farhat Salum, alisema tatizo hilo limesababishwa na damu kutozunguka
katika mkono wake.
Alisema
baada ya kuwekewa ‘kenyula’ katika mkono wake kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya
kifua cha nimonia,mkono wake ulikuwa unavimba.
Aidha
alisema baada ya kuona tatizo hilo
linaendelea muuguzi wa zamu alitoa taarifa kwa daktari kumuangalia kwa ajili ya
kupatia matibabu zaidi na kujua tatizo lake.
Alisema
baada ya daktari kufika alimwangalia na kugundua kuwa damu yake haitembei na
kumuita daktari wa upasuaji ili amuangalia zaidi na kushauri mkono ukatwe ili
tatizo lisiendelee kumuathiri.
“Kwa
kweli sio uzembe wa muuguzi wala daktari wa zamu bali ni tatizo la kiitaalamu
ambalo linaweza kumtokezea mtu yeyote na huyu mtoto limemtokezea wakati
alipotiwa ‘kenyula’ kwa ajili ya kuchomwa sindano matokezea yake limekuja
tatizo hilo ,”
alisema.
Aidha
lisema baada ya kupata taarifa hizo uongozi wa hospitali ulikaa pamoja na
muuguzi na daktari wa zamu wa siku hiyo na kulizungumzia tatizo hilo lakini
waligundua hilo ni tatizo la ‘gagril’.
Mbali
na hayo ameishauri jamii kuondoa dhana ya kuwepo uzembe wa muuguizi na daktari dhidi
ya matatizo yaliyomkumba mtoto huyo.
Hata
hivyo, alisema hali ya mtoto inaendelea vizuri na ugonjwa wa nimonia
unaomsumbua unaendelea kupatiwa matibabu na mkono wake unaendelea vizuri.
Mapema
mama mzazi wa mtoto huyo, Khadija Abdallah Salum, alisema mtoto wake alikuwa
nasumbuliwa na kifua cha nimonia na alipofika hospitalini aliandikiwa sindano.
Alisema
baadae mtoto wake alitiwa kenyula kwa ajili ya kuchomwa sindano lakini daadae
mkono ulianza kuvimba.
Alisema
baada ya kuona tatizo hilo alimuita muuguzi, lakini alimjibu kwamba mtu huanza kufa kuanzia miguu seuze huyo
mwanao huku akimwangalia mkono wake.
Alisema
baadae alimwita daktari kuja kumuangalia zaidi na kugundua kuwa mwanawe ana tatizo
na kumpeleka ICU na kukaa siku tano huku madaktari wakienda kumwangalia na siku ya Jumatatu walimwambia
kuwa mkono wa mwanawe haufai na utolewe ili sumu isienee zaidi.
Alisema
hivi sasa anaandikiwa dawa hizi na hizi na pesa hana na baada ya siku
hubadilishiwa dawa na kuambiwa hivi sasa usimpe hizi.
Ameiomba
serikali kumuangalia kwa jicho la huruma kwani yeye ni mnyonge na hana uwezo wa
kumuhudumia mtoto wake.
1 Comments
samahani sana lakini manesi na madakitari wetu ni jeuri sana , huwa hata mgonjwa akizidiwa ukimwita kumweleza wanakuwa hawana muda hata wa kukusikiliza , wakati mwengine wanatumia lugha za kukunyanyasa mpaka unaogopa hata kusema kitu mgonjwa akizidiwa , huu si ubinadamu , inabidi na wao watambue kuwa kuna siku watakuwa wagonjwa kama si wao basi vipenzi vyao , jee watakuwa tayari kufanyiwa hivo wanavyotufanyia sisi na watu wetu?
ReplyDelete