Na
Denis Mlowe, IRINGA
ASILIMIA
25 ya wanawake wako katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa saratani ya shingo
ya uzazi na kusababisha vifo kwa wanawake nchini.
Kwa
mujibu wa takwimu, asilimia 80 ya wagonjwa wanaobainika na aina hiyo ya
saratani, hugundulika wakati ugonjwa huo ukiwa tayari umeshasababisha athari
kubwa na kushindwa kutibika.
Hayo
yamebainishwa na Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu, wakati wa
uzinduzi wa mradi wa kuhamasisha jamii kuhusu huduma za uchunguzi wa saratani
ya shingo ya kizazi, uliondaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya T-Marc Tanzania .
Alisema
asilimia kubwa ya wanawake hawajitokezi kuangalia afya zao na kupima saratani,
hali inayosababisha ugonjwa huo kuongezeka.
Alisema
takwimu kutoka taasisi ya saratani ya Ocean Road, inaonyesha kati ya wagonjwa
wa saratani wanaopelekwa katika taasisi hiyo kila mwaka, zaidi ya wagonjwa 5,000
wana tatizo la saratani ya shingo ya kizazi.
Alisema
wataalamu wa mambo ya saratani wamegundua kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya
saratani ya mlango wa kizazi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Alisema
kutokana na tatizo hilo mkoani Iringa, serikali imewataka wadau kujitokeza
kuunga mkono ili kuhakikisha wanawake wanakuwa salama.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa T- Marc Tanzania,Diana Kisaka, alisema kila
mwaka wanawake 6,000 hugundulika na saratani ya mlango wa kizazi.
Alisema
wanawake 4,000 hufa kila mwaka nchini kutokana na saratani hiyo sawa na
wanawake 11 wanaofariki kila siku.
Alisema
takwimu za hospitali ya Ocean Road
zinaonesha asilimia 40 ya vifo
vinatokana na matatizo ya saratani ni wagonjwa
saratani ya mlango wa kizazi.
Alisema ugonjwa
huo ni tatizo kubwa ulimwenguni
na hasa katika nchi zinazoendelea ambapo takwimu za kimataifa zinaonesha kila mwaka zaidi ya
watu milioni 5 hugundulika na saratani
na kufanya tatizo hilo kufikia asilimia 29.
0 Comments