Bafana bafana kukata utepe na Cape Verde
WENYEJI wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2013, wamepangwa kufungua dimba la ngarambe hizo dhidi ya Cape Verde.
Hayo yamebainika baada ya droo ya kupanga makundi kufanyika juzi nchini Afrika Kusini.
Hafla ya kupanga makundi ya michuano hiyo, ilihudhuriwa pia na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Bafana bafana iko katika kundi A pamoja na timu za Angola, Morocco na Cape Verde.
Black Stars ya Ghana ambayo mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ilikuwa mwaka 1982, imepangwa na timu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Niger na Mali.
Mabingwa wa kombe hilo Zambia, wako kundi C pamoja na Nigeria, Ethiopia na Burkina Faso, huku Ivory Coast waliotinga fainali na Zambia wako kundi D na timu ya Togo, Tunisia na Algeria.
Tangu mwaka 2000, Cameroon wametwaa mara mbili kombe hilo, mwaka 2000 na 2002, wakati mwaka 2004 lilibebwa na Tunisia huku Misri ikilitwaa mara tatu kabla ya mwaka 2012, lilipokwenda Zambia.
0 Comments