Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji wa Benki ya Dunia (World Bank Managing Director for Operations) Bi. Anna Bjerde, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Marrakech, nchini Morocco, ambapo wamejadiliana kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Medium Term Review) utakaofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023, ukishirikisha wajumbe zaidi ya 250 kutoka mataifa takribani 100 duniani.
Rais Samia ashiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa
Afrika (AU) kuhusu Afya, Accra nchini Ghana
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan, akiwasili katika ukumbi wa mikutano, jijini Accra, Ghana kwa ajili
ya kushi...
2 hours ago




0 Comments